KUTANA NA BINTI ANAYETUMIA LAPTOP NA SIMU KWA ULIMI
Dhana ya mtu kuwa na ulemavu katika
maisha ndiyo kigezo cha kumfanya ashindwe kushughulika na jambo lolote
sio sahihi kabisa, kama ambavyo imekuwa ikithibitishwa na watu wenye
changamoto za ulemavu wa viungo kwa kufanya mambo makubwa na kuendelea
kufurahia wanachokifanya.
Ukiacha changamoto ambazo zinawakabili
watu hao, lakini bado wemeendelea kuwa mifano kwa watu wengine kama
ilivyo kila binadamu ana historia yake ambayo inaweza kumvutia mtu na
kumfanya ajifunze mambo mengi ambayo anaweza kuyatumia kama fursa katika
maisha ya kila siku.

Nursamawati Mahmud ni msichana mwenye
asili ya India ambaye anakumbwa na changamoto za kimaumbile kwa kuwa na
ulemavu wa miguu na mikono na kumfanya alazimike kutumia ulimi wake
pekee katika fanya mambo yake hususani matumizi ya LapTop na simu za
mikononi.

No comments:
Post a Comment
Comment here