Sherehe hiyo ilianza majira ya jioni ya jana saa 11,ambapo wahudhuriaji walipata fursa ya kusikiliza semina ya mfuko wa hifadhi ya jamii ya PSPF na baadae takribani wanafunzi wote walisajiliwa katika mfuko huo BURE kabisa ikiwa na pamoja na kupiga picha na ujazwaji wa fomu.viongozi na watu waliotoa mchango katika shughuli za MMUSO walitunukiwa vyeti na medali,baadhi ya watu hao ni lembrus mchome,baraka chitalilo,mboyi mkirya na n.k
Baada ya semina hiyo,majira ya saa 1 usiku,wahudhuriaji walipata chakula ili kujiandaa kwenda katika "session" ya usiku,huko sasa PALINOGAJE? unajua kilitokea nini?wacha nikujuze.Watu walipendeza sana kiukweli wake kwa waume asikwambie mtu.Kila mtu alijitahidi kuvunja kabati lake lake,kulikuwa na kosta mbili kwa ajili ya kuwapeleka mpaka eneo la tukio.
Wakati tupo kwenye moja ya kosta anbayo alipanda mwenyekiti wa sharehe hizo ndugu mboyi mkirya ,alifanya kama utani kwa kuwaambia watu mambo mbalimbali na moja jambo hilo ni kuacha kumuabisha kwa kutapika dagaa.
Mungu si baraka chitalilo,tulifika salama na pati ilianza kwa burudani ya mziki maridadi kutoka kwa dj maridaidi katika ukumbi huo.
MAMBO YA KUSIKITISHA KATIKA BAASH
- mboyi mkarya alipata matatizo ya kutapika
- neema swai alidondoka ukumbini
- na kuna mwanafunzi anafahamika kwa jina la kaunda,alimeza simu(hazijathibitishwa)
No comments:
Post a Comment
Comment here