Wednesday, December 23, 2015

HAWA NDIO WALIOKUSANYA MASHABIKI WENGI KWA MWAKA 2015 NCHINI TANZANIA

Mwaka ndio unaisha Ndugu yangu,lakini mbali na yote hapa Tanzania kuna watu mashuhuri ambao kwa mwaka huu walichukua headlines za kutosha katika media mbalimbali kama redio,runinga,magazeti na hata katika mitandao mbalimbali ya kijamii,kwa heshima na taadhima naomba niwalete kwenu hapa www.adamukihomile.blogspot.com


1.Diamond Platinumz
ndiye msanii pekee kutoka Tanzania ambaye ndiye kama amekuwa ni tishio kubwa kwa wasanii hata watokao nigeria,ndiye mmiliki wa hit song ya "nana"  ambayo imepatia tuzo nyingi za heshima.Pia amejaaliwa mtoto wa kike kwa mwaka huu aliyezaa na superstaa kutoka uganda,Zar  na kwa sasa anatamba na hit song nyingine ya utanipenda.
 



2.Edward Lowassa
alikuwa mgombea tishio wa upinzani wa URAIS wa tiketi ya chadema,alikihama CCM siku kadhaa baada ya kukosa uwakilishi wa urais wa chama hicho,baadae akajiunga na chadema kabla ya kukadhiwa kitambaa cha ukapteni na kuchukua fomu ya urais.

 
.

3.Millard Ayo
Ni mtangazaji wa clouds fm ya jijini dar-es-salaam,amekuwa zaidi ya mtangazaji maana tunaweza kumuita celebrity kwa sasa,anafanya kipindi cha ampifier na clouds top 20,lakini pia amenzisha studio yake binafsi#TZA#AYOTV ambayo imezidisha chachu na kumuongezea mashabiki kila kukicha.
 

4.Mbwana Samatta
ukitaja wachezaji bora wanaochezea hapa Afrika,huwezi kumuacha mshambuliaji huyu wa TP mazembe na timu ya Taifa ya Tanzania,ameingia katika orodha ya tuzo  mbalimbali za soka,na sitashangaa akienda kucheza soka ulaya 2016.
 

5.Salim Ahmed
mashabiki wa bongo movie wanamuita gabo zigamba,alianza na muhsin awadh(dk cheni),marehemu sajuki kabla ya kutambulishwa kabisa na jacob steven,jb katika filamu ya BADO NATAFUTA,lafudhi ya kimakonde,ana TV show yake inayoitwa BONDENI.

bado_natafuta

salim ahmed aliyekalia madumu.
endelea kutembelea blog hii kwa habari mbalimbali na motomoto ewe ndugu yangu kwa kuandika
www.adamukihomile.blogspot.com







No comments:

Post a Comment

Comment here