Muungano wa nchi wanachama wa Afrika
Magharibi ECOWAS umezitaka mataifa wanachama kupiga marufuku mtandio
unafunika hadi uso, ili kuzia mashambulio yanayotekelezwa na wanawake wa
kujitoa mhanga.
Mkutano wa ECOWAS uliofanyika mjini Abuja Nigeria
umesema mtandio huu wa hadi uso unayumbisha operesheni za maafisa wa
usalama katika kuwanasa wahalifu.Walipuaji wamekua wakivalia mavazi mapana na kuficha mabomu ndani ya mavazi hayo. Kundi hilo pia limetumia mbinu hiyo katika mataifa ya Cameroon, Chad na Niger ambayo yanashiriki katika operesheni dhidi ya Boko Haram.
No comments:
Post a Comment
Comment here