Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
ametua nchini Pakistan kwenye ziara ya kushtukiza ambapo anatarajiwa
kukutana na mwenzake Nawaz Sharif.
Bw Modi alikuwa safarini
kurejea India kutoka Afghanistan alipoamua kutua katika mji wa mashariki
wa Lahore. Ziara yake imelingana na siku ya kuzaliwa ya Bw Sharif.Bw Modi ndiye waziri mkuu wa kwanza wa India kuzuru Pakistan tangu 2004.
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili jirani, yenye silaha za nyuklia, ulikuwa umedorora kwa miaka mingi lakini sasa umeanza kuimarika.
Wawili hao walikutana kwa muda mfupi mjini Paris mwezi jana pembezoni mwa mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani wa COP21.
Mataifa hayo yamepigana vita mara tatu tangu kujipatia uhuru kutoka kwa Uingereza, vita vivili kuhusu jimbo la Kashmir.
Mataifa yote mawili hudai eneo lote la Kashmir, jambo ambalo yamezozania kwa zaidi ya miaka 60 sasa.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini mwaka 2003, lakini mara kwa mara kila upande hudai mwenzake ameukiuka.
No comments:
Post a Comment
Comment here