Makaburi matatu yanayotembelewa sana
na watu jijini Moscow yatawekewa huduma ya mtandao ya wi-fi.
Wanaotembelea makaburi hayo wataweza
kutumia mtandao wa intaneti bila malipo katika makaburi ya Novodevichy,
Troyekurovskoye na Vagankovo kuanzia mapema 2016 kwa mujibu wa tovuti ya Moscow
City.
Mkuu wa huduma za makaburi mjini
Moscow Artem Yekimov anasema lengo ni kusaidia wageni kwenye makaburi hayo
kutafuta habari zaidi kuhusu watu mashuhuri waliozikwa humo.
Aidha, kuwafanya wafurahie matembezi
yao makaburini.
Kampuni ya mawasiliano ya YS System
inasema ilijitolea kuweka huduma ya wi-fi humo baada ya kusikia mipango ya
kutenga maeneo ya watu “kutulia kisaikolojia” katika makaburi hayo.
Makaburi ya Novodevichy ni moja ya
maeneo yanayotembelewa sana na watalii Moscow.
Miongoni mwa watu waliozikwa humo ni
mwandishi Anton Chekhov, kiongozi wa zamani wa muungano wa Usovieti Nikita
Khrushchev na rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltsin.
No comments:
Post a Comment
Comment here