Watu wenye silaha wameshambulia chuo kikuu kimoja eneo la Charsadda kaskazini magharibi mwa Pakistan.
Washambuliaji
walijaribu kuingia ndani ya chuo kikuu cha Bacha Khan kwa nguvu na
makabiliano kati yao na maafisa wa usalama bado yanaendelea, ripoti
zinasema.Milipuko miwili mikubwa imesikika, afisa wa polisi ameambia shirika la habari la Reuters.
Ripoti zinasema watu wawili wamejeruhiwa. Maafisa wa usalama wamezingira chuo kikuu hicho.
No comments:
Post a Comment
Comment here