HIZI NDIYO SABABU ZA WANAWAKE KUTOPENDA WANAUME WAFUPI
Utafiti
nili usoma siku moja kuhusu wanaume wafupi, na walisema wanaume wafupi wana
mapenzi ya kweli na ya dhati kuliko wanaume warefu, kitu ambacho siwezi bisha
sababu, wanawake wengi huwa hawapendi kutoka na wanaume wafupi kwahiyo
inawachukua sana muda kupata mwenza na lazima wawapende na wawape mapenzi ya
kweli wanawake zao ili wasiwaache kwa sababu wanawake wengi wanapenda
mwanaume warefu na wengi wana mvuto kuliko wafupi.
Wanawake wengi wanapenda kutoka na wanaume ambao
wamewazidi urefu hata kidogo, kuliko kuwa na mwanaume ambaye ni mfupi kuliko
wao,wengi wanasema hii inaleta picha mbaya au muonekano mbaya wakiwa
wanaongozana wanaita (not Marching), lakini kuna sifa nyingine za wanaume
wafupi wanawake wengi wanasema zinawakera kama,
Wivu
Inasemekana wanaume wafupi wana wivu wa
kupindukia na sio kama wanaume wengine warefu hawana wivu ila wivu wao
unapitiliza kiasi cha kukera kwani wivu ukizidi sana ni kero katika mapenzi.
Wanaume wengi wafupi wana sifa sana, kiasi cha
kukera wanajisifia sana, na wanataka sana kuonekana, kama wapo eneo Fulani
wakiingia sehemu mtajua kama kuna mtu kaingia sababu ya sifa zao na maneno yao
japokuwa pia wana sifa moja ya kuwa wachechi sana.
Gubu
Hapa sasa ukichanganya na wivu ni balaaa maana
mwanaume mwenye gubu ni zaidi ya mwanamke muongeaji, Gubu ni ile hali ya
kukosoa kila kitu,kila kitu kibaya, yeye haridhiki na chochote na hata
utaonekana huwezi chochote akiwa karibu, hilo gubu au hata kama kila kitu kipo
sawa atatafuta sababu ya kuongea tu.
Wanajidai
Wanajua kila kitu. ( Much know)
Much knows, hapa bwana unakutana na mtu
kila kitu anajua yeye, ni kero sababu akiwa mbele za watu atataka kila
mtu ajue anajua nini kama inaongelewa siasa, mpira au mapenzi yeye fundi wa
kila kitu, kitu ambacho kiukweli kinakera sana wakati mwingine.
Muonekano/ Mvuto
Wanawake wengi wasema wanaume wafupi hawana
mvuto sana, kama wanaume warefu, kwahiyo hiyo ni moja ya sababu ya wao kutotaka
kutoka na wanaume wafupi, japokuwa sio wanaume wote wafupi hawana mvuto.
Japokuwa inasemekana siku hizi hakuna anae angalia urefu wako uzuri wako watu
wanangalia sana mfuko wako tu, hayo ni maneno ya mitaani watu wanaongea. Mimi
binafsi sijui kama ni hali halisi.
No comments:
Post a Comment
Comment here