Wimbo wa mwanamuziki Mwingereza Adele umevunja rekodi nyingine kwa kutazamwa mara bilioni moja haraka zaidi katika YouTube.
Video ya wimbo huo, Hello, imetazamwa mara bilioni moja katika YouTube siku 87 pekee baada ya kupakiwa kwenye mtandao huo.Wimbo huo umeupita wimbo wa Psy kwa jina Gangnam Style ambao ulitazamwa mara bilioni moja siku 158 baada ya kupakiwa. Wimbo huo ulichomolewa studioni Julai 2012.
Albamu ya tatu ya Adele, kwa jina 25, ndiyo iliyokuwa maarufu zaidi mwaka 2015 licha ya hali kwamba ilichomolewa studioni Novemba.
YouTube wanasema ni video 17 pekee ambazo zimetazamwa mara bilioni moja kwa sasa.
Video hizo ni pamoja na Sugar wa Maroon 5, Lean On wa Major Lazer, Love The Way You Lie wa Eminem, Party Rock wa LMFAO, Counting Stars wa OneRepublic, na Chandelier wa Sia.
No comments:
Post a Comment
Comment here