Friday, February 26, 2016

DIAMOND AWAJIBU HAYA WANAOSEMA AMECOPY VIDEO YA MAKE ME SING

Msanii mahiri anaeipeperusha vyema bendera ya Tanzania kutokana na uhodari wake wa kufanya kazi zinazo wavutia wadau wengi wa masuala ya burudani Nasib Abdul maarufu kama Diamond Plutnumz amefunguka kuhusu suala la video ya nyimbo ya pamoja kati yake na A.K.A ya Make Me Sing kufananishwa na video ya nyimbo ya Lil Wayne iitwayo Got Money

Akizungumzia suala hilo katika kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds FM Diamond ameeleza kuwa watu wanashindwa kuelewa,kila kitu ambacho kinafanyika sasa hivi kwenye muziki kuanzia video,mashairi vyote vilishafanyika.

Vyote vilishaimbwa,ni kama vinafanyika kwa marudio lakini kila mtu anarudia kwa namna yake anayoijua yeye,kwa sababu ukisema nakupenda watu washaimba,sikupendi washaimba vyote yaani, alisema Diamond

 

No comments:

Post a Comment

Comment here