WATOTO WAWILI WAMSHITAKI TB JOSHUA KWA KIFO CHA BABA YAO
Watoto
wawili wa Afrika Kusini wanamshitaki muhubiri wa kanisa kubwa na maarufu
nchinini Nigeria TB Joshua kwa kifo cha baba yao, wakili wao Bolajii
Ayorinde ameiambia BBC.
Watoto hao mmoja mwenye umri wa miaka
mitatu na mwingine wa miaka sita wamewasilisha nyaraka za mashtaka
katika mahakama ya mji mkuu wa Nigeria, Lagos, wakidai fidia ya zaidi ya
dola $521,000; kutoka kanisa la Synagogue Church of All Nations, vyombo
vya habari vya Nigeria vimeripoti.
Baba yao alikua miongoni mwa watu 116
waliokufa wakati jengo la makazi yanayomilikiwa na kanisa hilo
lilipoporomoka mjini Lagos mwaka 2014.
Mwaka jana mahakama ya uchunguzi wa vifo
iliamuru TB Joshua anapaswa kushtakiwa juu ya kuporomoka kwa jengo,
akisema kanisa hilo linahusika kwasababu ya uzembe wa kiuhalifu.
Muhubiri TB Joshua na kanisa lake wamekua wakikana kufanya kosa lolote.
No comments:
Post a Comment
Comment here