FID Q: TUSIMDHARAU CHID BEENZ
Rapa mahiri nchini Fareed
Kubanda maarufu kama Fid Q amefungukia suala la rapa anayefananishwa nae
kimichano maarufu kama Stamina kukanusha kujiita Chid Beenz.
Akizungumzia suala hilo katika mahojiano
yake na kipindi cha Planet Bongo ya East Afrika Radio rapa huyo amesema
hashangai watu kumfananisha na Stamina kimashairi na kuongeza kuwa kila
mtu anatambua kuwa Stamina amewahi kutangaza kufuata nyayo zake na
amekuwa akifanya hivyo kwenye nyimbo zake.
Akizungumzia suala la Chid Beenz rapa
huyo ameeleza kuwa bado anaamini uwezo wa Chid Beenz hivyo hakuna sababu
ya kumdharau kutokana na kupotea kwake kwenye game, huku akieleza kwa
jinsi anavyo amini uwezo wa Chid Beenz hakuna kinacho mshinda kwenye
staili ya michano.
No comments:
Post a Comment
Comment here