ndani ya wiki hii kwa hakika ndio stori iliyogonga sana vichwa vya watu hasa wanachuo wa MMU na wakazi wa ngaramtoni,kila mtu amediliki kusema lake kutokana na stori mbalimbali za mkasa huu chuoni hapa,lakini ufuatao ndio ukweli wenyewe.
MWANZO
adamu kihomile team ilifika mpaka eneo la tukio ambapo ni nyumbani kwa elimariki kambuga,ambaye ni rafiki mkubwa wa emmanuel khatibu ambaye huwa wanashikirikiana mambo mbalimbali na hata suala la kupika huwa wanapika pamoja.Siku hiyo kambuga alikuwa yupo chuoni lakini emma yeye hakwenda kabisa chuoni,MMU kutokana na sababu zake za msingi.
akiongea na mwandishi,mtu wa karibu wa emma na kambuga(jina limehifadhiwa),kwamba kwa kuwa kambuga hakuwa nyumbani kwake na wakati wa baadae kidogo emma naye alitoka,lakini huwa wanaacha funguo sehemu ambayo wanaijua wao tu(kambuga na emma) na hakuna mtu ajuaye.
baada ya muda kidogo kupita,akaja kijana mmoja mrefu huku akiwa anaongea na simu na kumkuta huyo mtu wa karibu wa kambuga na emma,"kambuga ameniagiza kompyuta yake nije kuichukua maana yeye yupo chuoni"alisema kijana huyo mrefu.
KUJUA FUNGUO ILIPO
yule kijana alisema mimi napajua ambapo funguo baada ya kuelezwa kwamba pamefungwa kwa kuwa hapakuwa na mtu yeyote ndani mle,basi akaingia na kuchukua hiyo kompyuta na kutoweka kusikojulikana.
BAADA YA KAMBUGA KUTOKA CHUONI
alipewa habari ya kuwa kuna kijana mrefu amekuja kuchukua hiyo kompyuta,yeye(kambuga) alihisi atakuwa ni sameer silvanus anayesomea bedgeo chuoni hapa,lakini alikana na kusema hakuchukua na hapo ndipo alipoanza kushtuka kwamba huenda ameibiwa.
SUALA LA KUHISIWA EMMA
kama nilivyowambia ndugu zangu ya kwamba emma ni rafiki mkubwa wa kambuga,na kwa kuwa alimuacha nyumbani wakati anaenda chuoni siku hiyo,alijua tu huenda ndiye aliyemfanyia unyama huo na kuamua kumpeleka "ngaramtoni police post".
BAADA YA KUFIKA POLISI
kwa kuwa hakutaka kuwa katika hali mbaya,emma aliamuaa kukubali ya kwamba ni kweli aliichukua ila atamlipa kidogo kidogo,chanzo kilisema.Lakini hali ilikuwa tofauti baada ya kufika nyumbani ambapo emma aliwaagiza wazee waongee na kambuga na kumueleza kuwa hakuiba hiyo kompyuta na alikubali pale pale polisi ili asiwe matatizoni.
MAAMUZI YA KAMBUGA
baada ya kuona kama analeta utani,kwa hasira hapo ndipo alipoamua kumrudisha tena polisi na mateso yalianza kumuandama kijana huyu.
lakini mule ndani(rumande)katika stori stori za hapa na pale,ndipo na emma alopoamua ku "share" stori yake.
KUFUMWA KWA DENIS OKWERA AKIUZA KOPYUTA
mmoja wa vijana waliokuwa lumande akamueleza emma kuwa,alimuona denis akiwa anatangaza kuuza kompyuta hiyo,sasa hapo wakapewa taarifa polisi na haraka sana wakaenda kumkamata denis na kumleta kituoni.
KUTAJWA KWA GEDION WA BEDMATH
denis baada ya kubanwa,akasema yeye si mwenye mali hiyo ila alikuwa dalali tu,alipewa na gedion huo mzigo.
JINA LA GEDION LAMPONZA GEDION
baada ya kutajwa gedion,hapo ndipo polisi wakaanza safari ya kwenda,bahati mbaya,wakaenga kwa gedion mwingine wa BEDGEO,gedion mhalu na ndipo mke wa denis akawaambia si yeye baada ya kufika polisi hapo,lakini alishapigwa sana na polisi na hapo ndipo walipomuamba radhi.
KUPATIKANA KWA KOMPYUTA
kwa kuwa denis ndiye dalali hivyo walienda mpaka walipouza na kupatiwa kambuga kompyuta yake,lakini mpaka sasa gedion wa BEDMATH hajulikani alipo.
TOA MAONI YAKO WEWE NDUGU YANGU,NI MUHIMU SANA
Pole gideon mhalu ,,,
ReplyDeleteHuwe fanya wiz mchiz wangu
Polisi mashost sometimes
Pole sana rafki angu Gideon mhalu,, kwa kuonewa
ReplyDeletePolice mnenepe akili sometimes sio mnapiga tu watu wasio nahatia ku*nina zen
Nhhhhhhh
ReplyDelete