MBINU ZA KUFUFUA PENZI LILILOKUFA
Mapenzi ni hisia zinazoumiza lakini
hazichoshi, hata uumizwe vipi huwezi kuacha kupenda, na katika maisha,
mapenzi yana nafasi kubwa sana
Tazama vikwazo,
Ni muhimu kujua nini vikwazo vilivyosababisha penzi lenu kuisha na
jitahidi kutatua hivyo vikwazo maana bila kufanya hivyo hautofanikiwa
kufufua mahusiano yako.
Amua kumpenda kama zamani,
Inabidi kutoka ndani ya moyo ukubali kumpenda kwa dhati na kumuonyesha mapenzi ambayo hapo nyuma hukuwahi kumuonyesha.
Omba msamaha.
Kubali kuomba msamaha hata kama kosa halikuwa lako kubali kujishusha
kwasababu wewe ndiye unaetaka mapenzi yenu yawe kama zamani.
Kurejesha mawasiliano,
Jitahidi kuboresha mawasiliano haswa mkiwa mbali ili kuweza kuleta ukaribu, kujua yuko wapi anafanya nini na nani.
Uaminifu,
Muamini kwa lolote atakalokwambia na usimfanye ahisi kwamba humuamini kwa sababu hiyo itasababisha kukukwepa msiwe mnaonana
Mazungumzo,
Ni muhimu kumkumbushia maisha ya zamani mliyopitia kipindi cha furaha na
epuka kumkumbushia mabaya mliyowahi kufanyiana kipindi cha nyuma.
Msifie,
Mfanye ajione kwamba yeye ni mzuri au handsome kwamba hujawahi kupenda
kama unavyompenda yeye pia ajue kwamba yeye ndo kitu bora zaidi katika
maisha yako.
Zawadi,
Mnunulie zawadi tofauti na sio lazima hizo zawadi ziwe za gharama ya juu
hata vitu vidogo vidogo vinaweza kuwa zawadi na mpenzi wako akafurahi.
Tenga muda kwa ajili yake,
Kutenga muda wa kumuuliza mambo yanayomuhusu yeye na hii itakusaidia wewe kujua wapi unafanya sahihi na wapi unakosea.
No comments:
Post a Comment
Comment here