UKWELI KUHUSU PENZI JIPYA LA SHILOLE NA MSANII HUYU WA BONGO FLEVANI
Post za Hitmaker wa Nyang’ang’a Zuwema
Mohamed maarufu kama Shilole na mwanamuziki chipukizi Nedy Music ambaye
yupo chini ya usimamizi mahiri wa meneja Mubenga, zimewafanya wadau wa
muziki kuhisi kuwa huenda kuna mahusiano kati yao.
Baada ya jitihada za kuwatafuta Nedy
Music na Shilole kugonga mwamba, mtembezi iliamua kupiga story na meneja
wa msanii Nedy Music, Mubenga ambaye ameeleza kuwa anazisikia taarifa
hizo kama watu wengine wanavyozisikia
“Nimezisikia
taarifa hizo kama watu wengine lakini nilipo jaribu kumuuliza Nedy
Music amekanusha kuwepo kwa mahusiano yake na Shilole, ila naimani
hawezi kunificha kitu” Alisema Mubenga.
Mubenga ameongeza kuwa hata kama
ikitokea Nedy Music akaja kutoka kimapenzi na Shilole hawezi kumkataza
kwani umri wake unaruhusu, ila mahusiano hayo yakiathiri kazi yake
ataingilia kati kwani kazi yake ni kufanikisha msanii wake anafanya
vizuri.
No comments:
Post a Comment
Comment here