Wednesday, May 11, 2016

Bidii kwenye kazi ! Bongofleva imempa Baraka Da Prince Lexus


Baraka Da Prince ni miongoni mwa wasanii wa kiume wa bongofleva ambao nyimbo zao zinachezwa sana kwenye Radio ambapo kwa sasa yuko mpaka kwenye Top10 na Top20 kupitia hit single ‘siwezi’
Ni miongoni pia mwa Wasanii waliopata mialiko ya kutosha kwenye show mbalimbali za Dar es salaam na nje ya Dar, kazi na jitihada zake zimeanza kumnyanyua kutoka kwenye hatua moja kwenda nyingine, na yeye anakua miongoni mwa Wasanii wenye magari yao binafsi.
Japokuwa hakupost picha zaidi ya moja ambayo inalionyesha gari hilo kwa ndani, Baraka aliandika kwenye Instagram yake maneno yafuatayo >>>Asante Mungu hiki kidogo na asante pia mashabiki kwa nguvu yenu na kuendelea kunisupport mziki wangu pamoja na media zote Tanzania

No comments:

Post a Comment

Comment here