HAMSINI KIKWAZO MABASI YA MWENDO KASI
Huduma ya Mabasi ya Mwendo Kasi imeanza
rasmi jana kwa abiria kulipa nauli elekezi huku ikikumbwa na changamoto
kadhaa ambazo zimesababisha kuwepo malalamiko kutoka kwa abiria lakini
uongozi wa mabasi hayo umesema unayafanyia kazi ili kupata ufumbuzi wa
kudumu.
Wakizungumza baadhi ya abiria wametoa
malalamiko yao wakidai kuwa wamefika kwenye kituo cha Ubungo muda mrefu
ila tatizo walilokumbana nalo ni kukosekana kwa chenchi ambapo
wanaokatisha tiketi wanadai chenchi ya hamsini ni ngumu kupatikana
kutokana na abiria kuwa wengi hivyo inawalazimu kuwataka abiria kuwa
wavumilivu ili waweze kuwatafutia.

Deus Mgawa ni Meneja Mahusiano wa UDART
amekiri kuwepo kwa changamoto hizo huku akidai kuwa watazifanyia kazi
kwa haraka ikiwemo kuharakisha kwa mfumo wa utumiaji kadi mfumo ambao
utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza foleni ya abiria katika ukataji wa
tiketi.
No comments:
Post a Comment
Comment here