JINSI UBUNIFU ULIVYOBADILI RAMANI YA BONGO FLEVA
Mziki wa Bongo Flava umebadilika sana,
kutoka kufanya Shoo za bure ili kujitangaza kama walivyokuwa wanafanya
wakongwe kama Prof. Jay hadi kufanya matamasha makubwa ya kulipwa kama
anavyofanya Diamond Platnumz na timu yake ya Wasafi.
Mabadiliko ya teknolojia yamechangia
sana ukuaji wa muziki wa Bongo Flava. Zamani uzalishaji wa mziki huu
ulitegemea waandaaji wawili wakongwe Master J na P-Funk Majani pekee,
lakini leo hii wasanii wanamiliki Studio zao kama Barnaba na studio yake
ya Hightable Sound au Dully Sykes na studio yake ya 4.12.
Soko la mziki limekua sana na hii ni
nzuri kwa kiwanda cha mziki Tanzania kwani inahitajika msanii kuwa
mbunifu na kujituma zaidi ili kuendelea kuwa bora. Hata kwa waandaaji
‘Producers’ ushindani umeongezeka sana kwani asipotengeneza mdundo mzuri
hawezi kupata nafasi ya kufanya kazi na wasanii wakubwa.
Kazi sasa imekuwa kwa Promota kuandaa
matamasha yenye hadhi ya kisasa ili waweze kutengeneza faida kubwa.
Malipo ya wasanii yamekuwa juu bila kuwa na maandalizi mazuri Promota
anaweza kuishia kumlipa msanii kisha yeye akapata hasara. Kizuri zaidi
kwasasa wasanii wengi wana uwezo wa kuandaa matamasha au Tour zao
wenyewe bila kutegemea Promota.
Haya ndio mabadiliko ya kweli kwenye Kiwanda cha Mziki Bongo ‘Bongo Flava’.
No comments:
Post a Comment
Comment here