Sunday, May 22, 2016

KILICHOJILI KATIKA BONANZA LA PSPF ARUSHA

kama hukupata nafasi ya kufika katika viwanja vya chuo cha IAA jijini Arusha ambapo ndipo bonanza la PSPF lilifanyika,nina mambo kadhaa yalifanyika nami sina budi kukuelezea

  • kulikuwa na michezo mbalimbali ambayo ilichezwa ikiwemo mpira wa miguu,kikapu,wavu na meza.
  • katika mchezo wa wavu,timu ya IAA iliibuka na ubingwa huo,ikifuatiwa na MAKUMILA,MMU huku SAUT ikishika mkia huo.
  • Na katika kikapu,timu ya MAKUMILA iliibuka na ushindi ikifuatiwa na ARUSHA UNIVERSITY, na IAA, na mchezaji nyoni talistu ndiye aliyeibuka kama mfungaji bora kwa upande wa kikapu.
  •  volleyball iliongozwa na MAKUMILA,IAA,MMU na wa mwisho ilikuwa ni chuo cha Arusha.
  • mpira wa miguu,mshindi ni IAA ikifuatiwa na SAUT huku kikundi bora cha ushangiliaji kikiwa ni cha IAA.
  • Pia kulikuwa na burudani ya muziki ambapo wanachuo mbalimbali walishiriki kuimba,baraka ngomas,blandii na sameer silvanus waliiwakilisha MMU katika tukio hilo ambapo baadae alipanda mrisho mpoto akiwa na bendi yake ya mjomba.
                       AHSANTE KWA KUISOMA HII

No comments:

Post a Comment

Comment here