LAKUZINGATIA UKITAKA KOLABO NA BARAKA DA PRINCE
Kushirikiana ni jambo la msingi sehemu
yoyote bila ushirikiano mambo hayawezi kwenda, kauli za Alikiba na
Diamond katika mahojiano mbali mbali walisikika wakisema kuwa msanii
akitaka”Collabo” lazima ajitathimini kwanza ndio wafanye “Collabo” hii
inathibitisha kuwa Collabo ina umuhimu mkubwa kwa msanii.
UFAFANUZI WAO
Kwanini wametoa kauli hizo?
walimaanisha kuwa msanii mchanga anapo taka ushirikiano katika nyimbo
lazima ajipange na uwezo binafsi sio pesa uwezo wake ndio utambeba ili
ngoma iwe kali, ikiwa msanii ana uwezo mdogo wanahofia kumfunika msanii
huyo na haita msaidia kwani lengo la msanii mchanga ni kutoboa katika
ramani ya muziki.
BARAKA DA PRINCE ANA YAKE
Kupitia Clouds Fm XXL amesema kuwa
anapata simu nyingi kwa wiki zinazo mtaka afanye Collabo inawezekana
asikubali hata moja kutokana na uwezo binafsi wa msanii wengine
wakimtaka wampe pesa ili wafanikishe ushirikiano huo hivyo ame waomba
wajipange kama maneno ya kaka zake .
Baraka Da Prince anatarajia kutoa
nyimbo aliyo mshirikisha Ali Kiba huku nyimbo aliyofanya na Mr Blue
pamoja na Ben Paul ziko hewani.
No comments:
Post a Comment
Comment here