Saturday, May 28, 2016

MADRID DERBY KUTIKISA JIJI LA MILAN LEO

Ni fainali ya michuano yenye msisimko mkubwa ya UEFA Champions League ambayo leo inafika tamati, vidume wawili kutoka nchi na jiji moja la Madrid yaani Real Madrid ya Zidane pamoja na Atletico Madrid ya Simeone nani kuchukua kombe hilo kwa mara ya kwanza? wewe unaishabikia timu ipi?

HISTORIA

Michuano hii ina umri wa mtu tena kwa aliyezaliwa miaka ya 1990’s inawezekana wakaiita babu michuano hii, ina miaka 61 yaani imeanzishwa rasmi 1955 kumbuka wazo la michuano hii limetoka kwa Santiago Bernabeu Yeste mwaka uliotajwa hapo juu yeye alianzisha michuano inayoitwa L’Equipe au Copa Latina, timu zilizokuwa zinashiriki kutoka Ufaransa, Italia, Ureno na Hispania ambapo baadaye ikabadilishwa jina na kuyaita UEFA CUP, miongoni mwa timu za awali kuchukua kombe hili ni Real Madrid, Benfica na Ac Milan.

BINGWA WA KIHISTORIA

Real Madrid ndiyo haswa bingwa mara nyingi wa michuano hii na ndio timu ya awali kuchukua kombe hili na amelichukua mara tano mfululizo wakati huo linaitwa UEFA Cup 1955 hadi 1960 kwa ujumla Madrid kachukua mara 10, kumbuka kuwa tangu lifanyiwe marekebisho 1992 hakuna timu iliyochukua mara mbili mfululizo.

ZINEDINE NA SIMEONE

Wote walikuwa wachezaji kipindi hicho na walicheza timu hizo wanazofundisha sasa na wamekuwa makocha wa timu hizo. Yoyote atakayechukua ataweka historia kwa kuchukua mara ya kwanza kwa upande wa makocha wakati kwa timu zenyewe Real Madrid wamechukua mara 10 wanasubiria historia ya kuchukua mara 11 wakati Atletico kama wakichukua itakuwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

Comment here