Sunday, May 8, 2016

Staa wa soka wa Misri na Tottenham aliahidi kufanya hivi, kama Leicester watakuwa Mabingwa

Ni wengi ambao hawakuwa na mawazo wala kuamini kuwa msimu huu klabu ya Leicester City itachukua Ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza kwa mara ya kwanza toka ianzishwe miaka 132 iliyopita, lakini wengi hawakuishia kutokuamini kwa mdomo wengine waliweka ahadi za kutekelezeka.


2012-634783924478878697-887
Ahmed Hossam ‘Mido’ enzi zake akicheza soka

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza na timu ya taifa ya Misri Ahmed Hossam ‘Mido’ ambaye sasa hivi ni mchambuzi wa masuala ya soka beIN Sports alikuwa ni moja kati ya watu wasiotarajia kuona hilo linatokea na kuhaidi kuwa kama Leicester watatwaa taji la EPL atanyoa nywele zake ambazo zimekuwa kama ndio utambulisho wake.

No comments:

Post a Comment

Comment here