SUMAYE:NASHANGAA KWA NINI RAIS MAGUFULI ANAPENDA SIFA
FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu
ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais John Magufuli kupenda kusifiwa
zaidi na kuchukia kukosolewa,
Sumaye bila kumtaja jina Rais Magufuli
ameleza kushangazwa na hatua ya serikali kuminya uhuru wa habari na
kwamba, kufanya hivyo kunalenga kuficha madudu yanayofanywa na watendaji
wake.
FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu
ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais John Magufuli kupenda kusifiwa
zaidi na kuchukia kukosolewa,
Sumaye bila kumtaja jina Rais Magufuli
ameleza kushangazwa na hatua ya serikali kuminya uhuru wa habari na
kwamba, kufanya hivyo kunalenga kuficha madudu yanayofanywa na watendaji
wake.
“Wapowatawala
ambao hawapendi kusemwa lakini wanapenda sana kusifiwa. Kiongozi mwenye
tabia ya udikteta hataki kusikia kingine zaidi ya sifa zake tu.
“Huyo ni mtu hatari na katika nchi ya
namna hiyo hakuna uhuru wa habari wala uhuru wa kutoa maoni kwa woga wa
kupotezwa kusikojulikana,” amesema Sumaye.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habri za Siasa
(TAPOREA), Sumaye amesema, serikali inakiuka Katiba ya nchi.
Amesema, serikali yoyote inayopambana
na vyombo vya habari na kuminya uhuru wa kufanya kazi zao huwa ina
tatizo kwa upande wa wanaotawala.
SOURCE:MTEMBEZI
No comments:
Post a Comment
Comment here