TAARIFA MPYA ZA MGOMO CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM)
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamegoma wakishinikiza Bodi ya Mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu.

Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi
chuoni hapo, Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa
zisizoeleweka zilizokuwa zikitolewa na Bodi ya Mikopo (HELSB) juu ya
lini fedha hizo zitatolewa.
Kama ilivyo ada fedha hizo za kujikimu
huingizwa kwenye akaunti za wanafunzi kila baada ya siku 60, lakini
mpaka sasa wanafunzi hao wanadai kuwa zimetimia wiki pasipo kuwekewa
chochote kwenye akaunti zao.
Mgomo huo unakuja zikiwa zimesalia siku mbili Rais Magufuli kuzuru chuo hicho kwa ajili uzinduzi wa Maktaba.
No comments:
Post a Comment
Comment here