USHOGA UNAZIDI KUENEA DUNIANI
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, ametoa pendekezo la kuhalalisha ‘ushoga’ na ndoa za jinsia moja nchini.
Akihutubia kwenye hafla ya maadhimisho
ya siku ya kupinga ubaguzi ulimwenguni, Pena Nieto alisema kwamba yupo
tayari kutia saini kanuni ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja nchini
humo.
Rais huyo pia alifahamisha kuandaa kampeni maalum ya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja na kufanyia marekebisho katiba kwa ajili ya suala hilo.
Kwa mujibu wa pendekezo la rais,
kipengele cha 4 cha katiba ya taifa ndicho kinacholengwa kubadilishwa
ili kuleta haki na uhuru wa ndoa za aina yote bila ya ubaguzi.
No comments:
Post a Comment
Comment here