Sunday, May 1, 2016

UTARATIBU WA BARUA ZA RESEARCH HUU HAPA


Imekuwa ni kawaida kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho kufanya utafiti (Research project) lakini katika kozi hii kuna utaratibu fulani lazima uufuate kwanza,nimekuletea utaratibu wote hapa ndugu yangu.

HATUA YA KWANZA

nenda katika ofisi ya mwalimu nzowa ili ukachukue barua ya utambulisho wa kufanya utafiti kutoka chuoni MMU ambayo itakuwa na saini ya dean.

HATUA YA PILI
unatakiwa uichukue hiyo barua na moja kwa moja utaipeleka katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambayo inapatikana arusha mjini karibu na jengo la EAST AFRICA COMMUNITY.

Ukiingia ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa,uliza chumba namba 5 ambapo ndipo wanapoipokea barua yako na utarudi kesho yake.

utakaporudi kesho yake,hutakiwa kurudi namba 5 tena,badala yake utaenda namba 9 ili uichukue.

HATUA YA TATU

unatakiwa uende katika ofisi ya mkuu wa wilaya,panda gari la USA RIVER na ushuke kituo kinachoitwa leganga hapo ukiulizia ofisi utafka kirahisi maana si mbali.


HATUA YA NNE
 baada ya mkuu wa wilaya,utapeleka katika ofisi ya mkurugenzi iliyopo sekei,hapo utakuwa umelimaliza zoezi lako.

TUKUTANE UWANJANI KESHO,NAIPENDA BED 3 TEAM WEWE JE????





No comments:

Post a Comment

Comment here