WABUNGE UKAWA NUSURA WAMPIGE MBUNGE WA CCM
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Jackline
Msongozi hivi karibuni amenusurika kipigo kutoka kwa wabunge wanawake wa
UKAWA baada ya kuwaeleza kuwa upande huo una wabunge wawili tu wenye
michango ya maana ambao ni Upendo Peneza (Viti Maalumu Chadema) na
Magdalena Sakaya (CUF).
Akichangia mjadala wa Bajeti kwa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Msongozi aliishambulia Kambi ya
Upinzani akieleza kuwa kuna mlevi mmoja amechangia upande wa upinzani
kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali wakati waliohusika na uuzwaji huo
wamehamia upinzani ambao ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Mara baada ya Bunge kuahirishwa wabunge
wanawake wa upinzani wakiongozwa na Sabrina Sungura na Ester Matiko
walimfuata Msongozi wakitaka kumshambulia, lakini aliondoka moja kwa
moja pasipo kusimama popote.
Sungura alipoulizwa alisema kuwa mbunge huyo angesimama wangemshughulikia.
No comments:
Post a Comment
Comment here