YANGA NA TUMBUA TUMBUA KAMA MAGUFULI
Mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya
makundi michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika mkondo wa kwanza
kati ya Yanga na Sagrado Esparanca ya Angola umemalizika kwenye uwanja
wa taifa na Yanga imeibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Mabadiliko yaliyofanywa na benchi la
ufundi la Yanga katika kipindi cha pili kuwatoa Malimi Busungu na Salum
Telela na nafasi zao kuchukuliwa na Geofrey Mwashiuya na Mbuyu Twite
yameisaidia timu hiyo kutoka mitaa ya Jangwani Kariakoo kuibuka na
ushindi.
Dakika ya 71 Msuva alifungua ukurasa wa
ushindi kwa kupachika bao la kwanza baada ya kupokea krosi kutoka kwa
Mwashiuya. Mchezo uliendelea kwa Yanga kushambulia lango la Sagrado
hadi dakika za nyongeza ambapo Matheo Antony alipiga shuti la
kushitukiza lililowababatiza walinzi wa Sagrado na kuingia nyavuni.
Filimbi ya mwisho ya mwamuzi kutoka
Ghana ili iruhusu Yanga kuondoka na ushindi wa mabao hayo 2 – 0. Kwa
ushindi huo Yanga imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele
kwenye michuano hii kwani itahitaji sare tu au isifungwe zaidi ya bao 1
kwenye mchezo wa marudio nchini Angola.
No comments:
Post a Comment
Comment here