ABDU KIBA KUTUA WCB?
“Nipo tayari naangalia pesa, kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo,”.
Kama umekuwa ukichanganywa na hicho
alichokiongea Abdu Kiba kuwa yupo tayari kusaini mkataba wa kufanya
kazi na lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kama hela itawekwa mezani,
basi usichanganyikiwe taarifa hizo ni za kweli na Abdu Kiba
amethibitisha kuwa aliyaongea hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano kwenye
kipindi cha Planet Bongo.
Baada ya
utata maneno hayo Abdu Kiba amelazimika kuvunja ukimya kwa kusema kuwa
mashabiki wamelipokea vibaya na kwamba hakumaanisha kama hivyo
lilivyopokelewa watu.
SWALI LA MSINGI:
Kama watu wamelipokea vibaya wewe ulimaanisha nini? yote ameyajibu
kwenye sauti hapo chini na kusisitiza kuwa hana mpango wa kuihama
menejimenti yake kwa sasa.
No comments:
Post a Comment
Comment here