HUYU NDIYE MBUNGE ASIYEJUWA KUSOMA WALA KUANDIKA KIINGEREZA
MLALAMIKIWA wa kwanza katika kesi ya
uchaguzi Jimbo la Longido mkoa wa Arusha, Mbunge wa Longido, Onesmo ole
Nangole (Chadema), ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuwa anajua
kusoma na kuandika Kiswahili, lakini hajui kusoma na kuandika
Kiingereza.
Shahidi huyo wa kwanza kwa upande wa
wajibu maombi, alisema hayo jana mbele ya Jaji Mfawidhi Kanda ya Bukoba,
Silvangirwa Mwangesi aliyesikiliza kesi hiyo wakati akihojiwa na Wakili
Dk Masumbuko Lamwai.
Wakili
Lamwai alitoa mahakamani hapo fomu iliyojazwa na Nangole, ambayo
ameiprint kutoka katika tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano ikiwa na
picha na kuiwasilisha mahakamani hapo, na aliomba kuisoma mbele ya Jaji
Mwangesi na inaonesha alisoma wapi mbunge huyo elimu ya sekondari.
Nangole aliisoma na kuonesha kuwa
alisoma katika Shule ya Arusha Sekondari mwaka 2008 hadi 2011, wakati
katika mahakama hiyo amesema hakusoma sekondari na wala hajui kusoma na
kuandika Kiingereza.
Wakili Lamwai alimuuliza Nangole kama
katika mikutano ya kampeni yeye na wafuasi wake, walitumia lugha za
kashfa dhidi ya mgombea wa CCM, Dk Stephen Kiruswa, ambapo alikana kutoa
lugha hizo.
Lakini, alipopewa hati ya kiapo chake
na kutakiwa kusoma, ilionesha kutamka maneno hayo katika mikutano ya
hadhara na katika kiapo chake. Nangole alipotakiwa kusema mahakama
iamini nini ili itoe maamuzi kwa kiapo alichoandika au alichosema
mahakamani hapo, Nangole alikaa kimya na Jaji Mwangesi alimwamuru kujibu
swali, ndipo aliposema hajui.
No comments:
Post a Comment
Comment here