PICHA ZA RAIS MAGUFULI AKIWA NDANI YA KOMBATI ZA JESHI
KUTOKA ARUSHA: PICHA ZA RAIS MAGUFULI AKIWA NDANI YA KOMBATI ZA JWTZ
Dk.
John Magufuli aliwasili mkoani Arusha jana ambapo kesho atakuwa
mgeni rasmi katika sherehe za kutunuku kamisheni kwa maofisa
wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha (TMA), Monduli.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix
Ntibenda, alisema Dk. Magufuli atawasili kupitia Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Kilimanjaro na amewaomba wananchi kujitokeza
kumpokea.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa
na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha TMA Meja Jenerali
PP Masao, Dk. Magufuli atatunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi
kundi la 57/15.
Alisema Dk. Magufuli atatunuku
kamisheni kwa maofisa wanafunzi kundi hilo, katika sherehe
zitakazoanza saa mbili asubuhi chuoni hapo.
Meja Jenerali Masao alisema wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo.
Hii ni ziara ya kwanza ya Rais
Dk. Magufuli ambaye pia ni Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya
ulinzi na usalama, kufika mkoani Arusha na pia kutunuku kamisheni,
baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo Oktoba, mwaka jana.
No comments:
Post a Comment
Comment here