Mke wa nahodha wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Wayne Rooney amejifungua mtoto mvulana.
Mtoto huyo amepewa jina Kit Joseph Rooney.Mwanasoka huyo alitangaza kuzaliwa kwa mtoto huyo Jumapili usiku kupitia mtandao wa Twitter, ambako anafuatwa na watu 12.5 milioni.

Mapema Jumatatu, alipakia picha ya mtoto huyo kwenye Twitter, baada yake kumuona mara ya kwanza, na kuandika: “Kukutana na Kit kwa mara ya kwanza. Twaenda nyumbani sasa”.
No comments:
Post a Comment
Comment here