Friday, June 3, 2016

ADHABU NYINGINE KALI KUTOKA KWA JPM

Baada ya jamii ya wakazi wa Kata ya Karansi, Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro kukubaliana kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno kuadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70, kali nyingine imeibuka baada ya Rais Magufuli kutembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba ya kisasa chuoni hapo.

Rais Magufuli ametoa kali nyingine baada ya kusema wanaopita kwenye barabara za mwendokasi zichomolewe tairi za magari yao kisha ziuzwe baada ya kupelekwa kituoni ili waharibifu wa barabara hizo nao wapate hasara kwa kuwa serikali iliingia gharama kubwa ya sh. bilioni 388 katika ujenzi wa miundombinu wa Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi.
“Mtu anapeleka gari lake humo anaondoka kule anazunguka humu wakati kuna barabara nyingine ipo kwa ajili yake, ‘no body is taking action’ … anatoka kule anampita traffic wala hamshiki na kwenda kulizuia gari lake likakae polisi, halafu siku akija kulichukua liwe halina matairi hatapita tena kwenye barabara ambayo hatakiwi, na akiuliza mbona halina matairi unamwambia lilikuja hivi hivi”
alisisitiza Dk. Magufuli.

Hivi karibuni Rais Magufuli alitoa kali nyingine baada ya kusema wafanyabiashara wote wanaoihujumu serikali yake kwa kuficha sukari ili wajineemeshe hata wafumbia macho, akasema “Nataka niwaambie sukari huwezi kuificha kama sindano, wafanyabiashara wote ambao wameficha sukari wale ni wahujumu uchumi; tutachukuwa sukari hiyo na tutaigawa bure na hawatafanya biashara maishani hapa Tanzania“.

No comments:

Post a Comment

Comment here