Friday, June 3, 2016

MATARAJIO YA KUSAINI PESA YA KUJIKIMU KWA WANACHUO YANAKUJA


kumekuwa na hali ya sintofahamu kuhusiana na pesa ya kujikimu wanachuo (boom) katika vyuo mbalimbali ambapo pesa hiyo hutolewa kila baada ya siku 60,na kwa mujibu wa kalenda ya bodi ya mikopo siku 60 zao zinaishia kesho.

Akiongea na adamukihomile.com,waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi wa MMU  amesema kuwa,matarajio yao siku ya kesho pesa za wanachuo hapa MMU zitawekwa katika akaunti kwa ajili ya kupewa wanafunzi pesa zao.

Aidha aliongeza kuwa na kama hazitawekwa kesho,basi itakuwa tarehe 11 kwani pia bodi ya mikopo ina tabia kuwahi au kuchelewa kwa siku 7,hivyo basi kuhusu kusaini  wanachuo zao,itategemea na ni siku ipi pesa itaingizwa kwenye akaunti,kama itawekwa tarehe 4 yaani kesho,basi wanachuo watasaini jumatatu ya  tarehe 6 na kama itawekwa tarehe 11,pesa itasainiwa na wanachuo tarehe 13.

pia waziri amewakumbusha wanachuo wa MMU kuwa tarehe  17-20 ,maofisa wa bodi ya mikopo watakuwepo chuoni hapo na kila mwanafunzi anapaswa kuwepo katika zoezi hilo akiwa na kitambulisho cha chuo na "passbook yake ".
 
                                               #AHSANTE KWA KUISOMA
  .

No comments:

Post a Comment

Comment here