HAWA NDIO MABEKI 10 VITASA KWENYE MICHUANO YA EURO2016
Moja ya nafasi muhimu uwanjani ni sehemu
ya ulinzi. Hii ni muhimu kwa timu yoyote ya mpira wa miguu ili iweze
kupata ushindi ni lazima ukuta wao uhakikishe unazuia mashambulizi ya
timu pinzani.
Kuelekea michuano ya EURO2016 nchini
Ufaransa leo tupate wasaa wa kutazama mabeki kumi bora wanaotarajiwa
kufanya makubwa na kuzisaidia timu zao za taifa.
10. Jose Fonte: Huyu ni mlinzi wa kati
raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 32 na amekuwa na msimu mzuri ndani ya
Southampton hivyo atakuwa kwenye ukuta wa Ureno akiwasaidia Louis Nani
na Ronaldo kuhakikisha wanashinda.
11. Stephan Lichtseiner: Ni beki wa
kulia wa Juventus na Timu ya Taifa ya Uswisi. Naye atakuwepo kuhakikisha
nchi yake inaondoka na ubingwa wa Ulaya.
12. Sime Vrsaljiko: Ni mlinzi wa kati wa
Klabu ya Napoli na Timu ya Taifa ya Croatia. Atakuwa anawakilisha taifa
lake na Ivan Rakitic pamoja na Luka Modric.
13. Toby Alderweireld: Raia wa Ubeligiji
na beki wa kati wa Tottenham. Amechukua nafasi ya Vincent Kopany hivyo
atakuwa akina Eden Hazard na Kevin De Bruyne kuhakikisha kombe linaenda
kwao.
14.Elseid Hysaj: Ni raia wa Albania
anayekipiga Napoli kama mlinzi wa kati naye ni moja ya nyota
wanaotarajiwa kufanya vizuri EURO2016.
15. Juanfran: Nyota wa Hispania na
Atletico Madrid naye yumo katika walinzi kumi wanaotajiwa kufanya
vizuri. Anakumbukwa kwa kukosa penati kwenye mchezo wa fainali ya Uefa
dhidi Real Madrid na kuikosesha ubingwa timu yake.
16. Mats Hummels: Ilikuwa roho ya
Dortmund lakini tayari imenyakuliwa na Bayern Munich kwa ajili ya msimu
ujao. Atakuwa anaongoza ukuta wa Ujerumani kuhakikisha wanatwaa ubingwa
huo.
17. David Alaba: Ni kipenzi cha Pep
Guardiola akiwa na uwezo wa kucheza kama kiungo ama winga, japo hucheza
sana kama mlinzi wa kushoto. Atakuwa na kikosi cha Austria wakisaka taji
la EURO2016.
18. Sergio Ramos: Ni mlinzi wa kisasa
anayejua kufunga pale inapobidi afanye vile na hapo ndipo anakumbukwa
vizuri kwa kufunga kwenye fainali mbili za Uefa zote dhidi ya Atletico
Madrid. Atakuwa na kikosi cha Hispania wakisaka taji la Euro kwa mara ya
nne.
19.
Leonardo Bonucci: Raia wa Italia anafahamika kama mtaalam wa ‘Tackles’.
Anakipiga Juventus na atakuwa na timu yake ya Italia nchini Ufaransa
wakipambana kusaka ubingwa wa EURO2016.
Hao ndio walinzi wanaotarajiwa kuzitetea timu zao kwenye michuano inayoanza June10 nchini Ufaransa.
No comments:
Post a Comment
Comment here