PAPA FRANSIS APITISHA SHERIA MPYA KANISA KATOLIKI
Kiongozi
wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Fransis ametangaza kuwa
maaskofu wa kanisa hilo watakaoshindwa kushughulikia makasisi
waliokumbwa na hatia ya kuwanyanyasa kingono watoto wadogo wanaweza
kuondolewa katika madaraka yao.
Sheria
mpya ya Vatican iliyotolewa na Baba Mtakatifu Jumamosi inaonekana kuwa
ni majibu yaliyotafutwa muda mrefu na wanaharakati wa kikatoliki nchini
Marekani ambao walipinga walichokiona ni kushindwa kuchukuliwa hatua
dhidi ya makasisi waliotenda uovu huo.
Agizo la Baba Mtakatifu limeweka wazi
kwamba hata wale maaskofu ambao hawashutumiwi kuwanyanyasa kingono
watoto wanaweza kuondolewa kwenye nafasi zao kama wataonekana
wameshindwa kuchukua hatua na kulinda waumini wao kutokana na manyanyaso
ya mapadri.
Maaskofu tayari wanauwezekano mkubwa wa
kuwajibishwa au kupoteza nafasi zao za kazi kama sababukuu
zitathibitishwa. Waathiriwa wa manyanyaso hayo nchini marekani na
kwingineko duniani kwa muda mrefu wamelalamika kwamba baadhi ya maaskofu
wanapuuzia au kuficha vitendo vya unyanyasaji ndani ya kanisa.
Chanzo: VOA Swahili
No comments:
Post a Comment
Comment here