NJIA ZA KUDUMU NA MPENZI WAKO ALIYE MBALI
Siku zote mapenzi huyapa maisha thamani
lakini wapo ambao hujikuta kwa namna moja ama nyingine wanatengana na
wapenzi wao kwa sababu tu ya mihangaiko ya kila siku ya kujitafutia
riziki au masomo na wakati mwingine utengano huwa ni matokeo ya
wapendanao kuishi sehemu tofauti.
Umbali hulifanya penzi baina ya
wapendanao kuteteleka kama wapendanao hawatafanya kazi za ziada
kuhakikisha wanaziba mianya yote itakayosababisha usaliti kama sio
kuachana kabisa, hata hivyo, mapenzi ya mbali huna ni vigumu kuteteleka
endapo tu wapendanao wanamapenzi ya dhati na kutamani kuwa pamoja kila
wakati na mmoja wapo kuamua kujitoa muhanga kwa kuamia anakoishi ama
anakofanyia kazi laazizi na mwandani wake.
Pamoja na hayo yote bado umbali hauwezi
kuwa ni tatizo kubwa sana la kutetelesha uhusiano wako na mpenzi wako,
Mnaweza kudumisha mapenzi yenu ya mbali endapo utafanya haya
1.MAWASILIANO MARA KWA MARA
Mawasiliano ni nguzo muhimu sana baina
ya wapendanao, humfanya kila mtu kuhisi uwepo wa mwenzi wake hata kama
atakuwa mbali naye. Hivyo, kama una mpenzi wako aliye mbali nawe
hakikisha unakuwa naye karibu kwa kumtumia sms, email, kadi au simu,
Aidha, pindi mnapowasiliana hakikisha humkwazi mwenzako kwa namna yoyote
ile.
2.HESHIMU HISIA ZAKO
Mapenzi ya kweli yametawaliwa na hisia
kali ambazo ndizo huwafanya wapendanao kufikishana kwenye mambo fulani
kwani pasipo hisia hata uwe na ujuzi au utundu wakutosha hutapata raha
ya mapenzi, Kama kweli unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana
kutokana na sababu za kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari
kumtunzia penzi lake hadi mtakapokutana tena.
3.UMBALI ISIWE KIGEZO KUNYIMANA
Mpe mwandani wako raha kamili kama
ilivyokuwa awali mlipokuwa pamoja! Bila shaka unajiuliza inawezekanaje?
Hili linawezekana kwa kutumia njia yoyote ya mawasiliano. Mfano kama
nyote mna simu jiandae vya kutosha nikiwa na maana uhakikishe upo sehemu
ambayo utakuwa huru kuongea ama kufanya chochote Kitakachokufanya uhisi
raha isiyo na kifani na kukufikisha kwenye kilele cha mlima kilimanjaro
bila kutarajia.
No comments:
Post a Comment
Comment here