Washia ndio wachache Nigeria lakini
idadi yao imekuwa ikiongezeka karibuni
Waislamu wa dhehebu ya Shia
kaskazini mwa Nigeria wameandamana kupinga operesheni wa kijeshi ambayo
wanasema ilisababisha vifo vya mamia ya waumini.
Maandamano yalishuhudiwa katika miji
sita mita mikuu, mji wa Kaduna ukiathirika zaidi.
Rais wa Iran, Hassan Rouhani
alimpigia simu mwenzake wa Nigeria Muhammadu Buhari kuhusu operesheni hiyo ya
jeshi.
Iran ni taifa la Kishia.
Jeshi la Nigeria linatuhumu dhehebu
hilo la Kishia kwa kujaribu kumuua mkuu wa jeshi Jenerali Tukur Buratai.
Dhehebu hilo kwa jina Islamic
Movement of Nigeria (IMN), limekanusha madai hayo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya
Iran, kwenye mawasiliano yake na Bw Buhari, Bw Rouhani aliuliza kuhusu hatima
ya Sheikh Ibraheem Zakzaky, kiongozi wa IMN aiyekamatwa baada ya wanajeshi
kuzingira nyumba yake katika mji wa Zaria.
Dhehebu la IMN linasema mamia ya waumini
wake waliuawa na wanajeshi na madhabahu ya kundi hilo yakaharibiwa kwenye
operesheni ya kijeshi.
Mtetezi wa haki za kibinadamu Chidi
Odinkalu, ameunga mkono takwimu zinazotolewa na kundi hilo na kumtaka Rais
President Buhari kuunda tume huru ya uchunguzi
“Haiwezekani. Wanigeria wana haki ya
kuishi. Jeshi linawezaje kukabili watu wanaoandamana wakirusha mawe kwa
bunduki?” Bw Odinkalu ameongeza.
Jeshi
limesema linamzuiliwa Sheikh Zakzaky
Kundi la IMN lina makao makuu yake
IMN na wafuasi wa dhehebu hilo waliandamana, huku vikosi vya usalama vikishika
doria.
Mwandishi wa BBC Nura Muhammed
Ringim anasema watu wengi walisalia manyumbani wakihofia usalama.
Miji ya Kano, Katsina, Sokoto,
Zamfara na Bauchi pia ilishuhudia maandamano.
Nchini Iran, kundi la watu
lilikusanyika nje ya afisi za Umoja wa Mataifa mjini Mashhad kupinga maandamano
hayo, kwa mujibu wa shirika la habari la kibinafsi la Tehran Tasnim.
Jeshi halijatoa idadi ya watu
waliofariki, lakini limekanusha madai kwamba mkewe kiongozi huyo wa IMN Zeenat
Ibrahim aliuawa.
Meja Jenerali Oyebado, mkuu wa jeshi
wa Kaduna, alisema Jumatatu kwamba mwanamke huyo anazuiliwa na jeshi.
Hakuthibitisha wala kukana madai ya
kuuawa kwa mwana wa kiume wa Sheikh Ibraheem Zakzaky, Sayyid Ibraheem Zakzaky.
Mwaka uliopita, wana watatu wa kiume
wa Sheikh Zakzaky waliuawa kwenye makabiliano kati ya jeshi na wafuasi wa
dhehebu hilo.
No comments:
Post a Comment
Comment here