KIPA WA SIMBA ANAYESUGUA BENCHI KWA AJILI YA MAPENZI
Baada ya kuona kipaji cha mwanae
kikipotea wakati akiwa na kazi kubwa ya kulitumikia taifa lake, Baba
mzazi wa kipa wa klabu ya Simba, Peter Manyika Jr, Manyika Peter
ameibuka na kumkoromea mwanae.
Baba mzazi huyo alisema kinachomponza mwanae ni kukosa nidhamu na pia kutekwa na mahusiano ya kimapenzi aliyonayo kwa sasa.
Akizungumza kwa uchungu, nyota huyo wa
zamani wa Sigara, Mtibwa Sugar, Yanga na Taifa Stars, alisema mwanaye
anapotea kwa sababu ya kuendekeza starehe na huwa anajisikia vibaya
anaposikia akiwajibu mbovu waanahabari na hata viongozi wake kuhusiana
na sakata lake la mambo ya mapenzi.
“Amesajiliwa
Simba afanye kazi siyo kula mshahara wa bure na kuishia kukaa benchi,
viongozi hawana tatizo kama angekuwa msaada angepangwa lakini yeye
ajiulize na hayo mahusiano aliyonayo kama yanamsaidia katika kazi yake?” Alihoji bila kumuweka hadharani binti huyo anayemzingua Manyika
“Akipata
jibu na atarudi kwenye mstari, kama mzazi najisikia uchungu sana kwa
yale anayoyafanya mtoto wangu kwa sababu najua maisha ni nini lakini
yeye anaona mjanja ila nina shaka hapo mbele asije akaumizwa vibaya,” alisema Mzee Manyika.
Aliongeza, “Nimecheza
nafasi kama yake kwa mafanikio makubwa, ndiyo maana nasema kwa uchungu
kwamba jibu ni mwanangu wala siyo viongozi yeye ndiye chanzo kwa sababu
wasingeweza kutupa pesa yao bure kumsajili kwa mkataba wa miaka mitatu
kama pambo bali kwa ajili ya kufanya kazi yao,”
Pia alisema kuwa hawezi kumkataza mwanae
kuendelea na mapenzi na mwanamke aliyenaye, isipokuwa ni vema kuangalia
mustakabali wake kwa sababu mtaji wake ni kipaji cha soka na akizembea
atakuja kujuta mbeleni.
“Kipindi
nilichokuwa nacheza na staa katika jamii nilifuatwa na wanawake wa kila
aina na wengine kutaka wagharamikie kwa kila hali lakini nilikuwa na
msimamo na kupuuza mambo yao na sitaki mwanangu aangamie,” alisema Manyika.
Kipa Manyika aliposakwa kwa njia ya
simu, hakupokea simu aliyopigiwa, lakini kocha wa makipa wa Simba Adam
Abdallah, alisema kinachofanya Manyika Jr, asugue benchi ni kutokana na
kukosa nafasi mbele ya Vincent Angban aliyepo juu kwa sasa lakini
mchezaji huyo si mbaya.
No comments:
Post a Comment
Comment here