Saturday, March 12, 2016

WALIOKUMBWA NA MIKASA YA WIZI MMU HAWA HAPA







Katika jamii yoyote ile katika maisha ya wanadamu,aidha shuleni,maofisini,nyumba za ibada na hata vyuoni,suala la wizi limekuwa limeshamiri kwa kiasi kikubwa sana,ukienda vyuo vikubwa kama UDSM,UDOM na vinginevyo,suala hili limekuwa ni gumzo na ni changamoto kubwa,hivyo basi,leo nimeamua kukuletea orodha ya wanafunzi ambao mkasa wa wizi hapa chuoni MMU umeshawatokea:
·         Abdallah kambenga
ni mwanafunzi mcheshi sana kimuonekano,anapenda sana kwenda na muda kwenye mambo yake,lakini hayo yote hayakuweza kuzuia kuibiwa kopyuta mpakato “laptop” zake mbili.
Cha ajabu zaidi,moja ya kompyuta yake wakati anaibiwa,mwizi aliiba hiyo laptop alafu siku ya pili yake akaja kumalizia chaja yake,hakuzipata.
·         Elimarik Kambuga
Takribani wiki nzima ndio imekuwa kama stori ya MMU,na wengi waliipata,kambuga ni mtu maarufu sana lakini mwisho wa siku ndio hivyo tena aliibiwa laptop yake,aliipata.
·         Chite
Ukiwa ni mtu wa karibu na kijana huyu,ni lazima utapata fursa ya kuona alama ya kovu,si nduwi ile,ila ni moja ya majeraha aliyoyapata katika zile purukushani za hapa na pale wakati wa uvamizi  wa majambazi katika hosteli(jina limehifadhiwa) ambayo alikuwa anaishi,vitu vingi vilichukuliwa usiku ule,watu kama lymo walipata madhara hayo.
·         Jumanne
Anasoma shahada ya elimu katika masomo ya uchumi,aliibiwa wakati anatoka kwake ili aende msikitini,kwa bahati mbaya alisahau kufunga mlango hivyo vitu kama laptop na smartphone yake vilichukuliwa,hajavipata.

JE,UNAMFAHAMU MHANGA MWINGINE WA WIZI HAYUPO HAPA,COMMENT HAPA CHINI TAFADHALI.

No comments:

Post a Comment

Comment here