MR.BLUE: NGOMA YANGU NA ALI KIBA ITAACHA HISTORIA
Hitmaker wa baki na mimi ambaye hivi
karibuni aliuaga ukapera kwa kuamua kufunga pingu za maisha na mzazi
mwenzake Wayda, ameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia kolabo yake na
msanii nyota kwa sasa Alikiba aliyoipa jina la Mboga Saba.
Akizungumza na adamukihomile.com
Mr. Blue amesema kuwa ngoma hiyo ipo tayari na anatarajia kuiachia wiki
ijayo endapo mtayarishaji wa ngoma hiyo Man Water atamkabidhi, hivyo
itakuwa rahisi kwake kuikabidhi kwa mashabiki wake.

Blue ameongeza kuwa Mboga Saba ni ngoma
ya aina yake ambayo anaimani itapokelewa vizuri na mashabiki wake kwa
kuacha historia ya ngoma alizowahi kuzifanya, kwani wote wawili
wameonesha umahiri mkubwa, katika hatua nyingine Blue amesema mashabiki
wake wajiandae pia kwa ngoma mpya ya kundi lake la B.O.B Micharazo
ambayo ameirekodi kwa Man Water.
No comments:
Post a Comment
Comment here