MSHAMBULIAJI NYOTA EPL AKIRI KOSA HILI
Mshambuliaji wa vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester City Jamie Vardy amekubali mashtaka ya utovu wa nidhamu.
Vardy mwenye umri wa miaka 29
alimkaripia mwamuzi Jon Moss baada ya kufukuzwa uwanjani kwa kadi
nyekundu wakati wa mechi ya Jumapili ambayo walitoka sare 2-2 na West
Ham.
Kwa kukubali shitaka hilo la Shirikisho
la Soka la Uingereza (FA), Vardy, ambaye alikuwa ameitisha kikao cha
kujitetea, huenda akaongezewa adhabu juu ya adhabu ya sasa ya
kutoruhusiwa kucheza mchezo mmoja.
No comments:
Post a Comment
Comment here