Friday, April 29, 2016

PAPA WEMBA ALISHATABILI KIFO CHAKE

Papa Wemba mfalme  wa muziki wa  Lese Rumba  almaarufu kama ‘Soukous’ alietamba miaka 1969  na Bendi maarufu ya ‘Soukous’ Zaiko Langa Langa amekuwa Simba ambaye inaaminika ndiye mfalme wa mwituni kwa kukamilisha mawindo yake kishujaa baada ya kufanikisha kile alichotamani kitokee katika maisha yake ya Muziki wa Rumba nchini Kongo.

 

Amewahi kunukuliwa na baadhi ya Vyombo vya Habari akisema kitu anachotamani kitokee katika kukamilisha safari yake ya muziki hapa duniani ni kufia stejini kwani ndio sehemu pekee ambayo hujihisi kama anapaa akiwa anaimba.

“Nataka nifie stejini, nataka siku zangu za mwisho ziwe jukwaani kwa sababu kila muda ninapokuwa jukwaani nikiimba nahisi kama ninapaa”.

Ama kwa hakika sisi sote  viumbe wa Mungu na kwake tutarejea; alichokitabiri Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba almaarufu kama Papa Wemba kimetimia Aprili 24 mwaka huu alipokuwa Abidjan nchini Ivory Coast wakati akitumbuiza katika Tamasha la Festival des Musiques Urbaines d’Anoumabo (FEMUA)

 mwili wa Papa Wemba umewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kinshasa tayari kwa maziko .

No comments:

Post a Comment

Comment here