Friday, April 29, 2016

USIMLINGANISHE NA MESSI

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amesema kamwe Saul Niguez asifananishwe na Lionel Messi baada ya Atletico Madrid kuibuka washindi wa mechi ya mkondo wa kwanza nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.1

 

Saul alifunga bao la aina yake baada ya kuichambua ngome ya Bayern kisha kufunga na baada ya mechi alianza kulinganishwa na supastaa wa Barcelona Lionel Messi, aliyefunga magoli mengi kwa kuwachambua mabeki.

Hata hivyo, Guardiola amesema ni vema kutomlinganisha nyota huyo wa miaka 21 na nahodha wa Argentina. “Binafsi simjui vizuri, lakini naheshimu ubora alionao Saul,” alisema. “Lakini itakuwa vema kwake kutomlinganisha na Messi.”

No comments:

Post a Comment

Comment here