ATHARI ZA KISAIKOLOJIA ZINAZOMKUMBA MTOTO ANAYELELEWA NA MZAZI MMOJA

Mzazi mmoja ni nani? ni mtu ambaye amefiwa na mume au mke na kuachiwa malezi ya watoto peke yake.
Pia mzazi mmoja anaweza kuwa mwanamke au
msichana aliyepata ujauzito bila kufunga ndoa, hapa anaweza kuwa
mwanafunzi wa sekondari, shule ya msingi au wa Chuo Kikuu.
Pia kwa maisha ya siku hizi wanawake
wenye uwezo kimaisha hupendelea kulea watoto wao bila msaada wa mwanaume
aliyezaa naye kwani wengi wao hukwepa kuingia kwenye maisha ya ndoa kwa
sababu mbalimbali.
ATHARI ZA KISAIKOLOJIA
Uchunguzi uliofanywa na wanasaikolojia
umebaini kuwa mtoto mwenye umri kati ya miaka mitatu hadi mitano hasa wa
kiume huwa karibu sana na mama na watoto wa kike wenye umri huo pia
huwa karibu zaidi na baba, kutokana na ukaribu huo watoto hao watakuwa
na mapenzi hata wakija kuingia kwenye mahusiano pale wanapokuwa
wamevunja ungo au kubalehe hukosa uelekezi mzuri kwenye tabia chanya.
Kukosa ukaribu; watoto
hasa kwenye kipindi cha kubalehe au kuvunja ungo ndio athari zinaanza
kujionesha kwani kuna vitu ambavyo anatamani kumueleza na mzazi husika
kama ni baba au mama ili kuweza kupata taarifa husika, lakini pale
anapokosa maelekezo ya mzazi ananza kutafuta taaarifa kutoka kwenye
mitandao ya kijamii ambayo itamsababisha kutopata uhalali wa jambo
analotarajia kulifahamu.
Athari ya kiuchumi; hapa
anazungumziwa mzazi asiye na uwezo wa kutimiza mahitaji ya mwanae
kutokana na kudorora kwa uchumi ambapo hupelekea mtoto kuathirika
kisaikolojia kwa kukosa mahitaji muhimu shuleni kama viatu, sare za
shule na ada. Hali hii inayompelekea unyonge mtoto huyu kitaalamu huitwa
(Inferiorty Conflict) ambayo huathiri namna ya kujifunza.
Kupata kasoro za kisaikolojia kwenye jamii; hapa
mtoto ambaye anapata malezi ya mzazi mmoja anakosa kujiamini hata mbele
za watu kwani hakupata malezi ya pande zote mbili hali inayochangia
kufifisha uwezo wake wa kujiamini.
No comments:
Post a Comment
Comment here