wanachuo wa mount meru university-MMU
Karibu sana mpenzi msomaji wa blogu hii,Leo hii tutakuwa na
somo jepesi sana kwa wanafunzi na wanachuo la kujifunza ni namna gani tunaweza
kuzikokotoa GPA zetu kupitia masomo
tuyasomayo,haya sasa naomba tufuatane kuanzia mwanzo hadi mwisho ndugu yangu.
a)
Jambo la kwanza la kutambua ni kuelewa kila
daraja linabeba pointi ngapi katika kutafuta GPA.
Daraja A pointi 5,B+ pointi 4,B pointi 3 na
daraja C lina pointi 2.
b)
Unakumbuka zile hesabu za kutafuta wastani? Kama
umesahau basi ni hivi,ukitaka wastani wa namba kadhaa mfano 1,2,3 na 4 huwa
tunachukua jumla ya namba (1+2+3+4)=10 ambayo tunagawanya na idadi y namba
ambazo zipo 4 hapa tukigawanya tutapata
2.5 (yaani 10 gawanya kwa 4)
c)
Sasa basi baada ya kujikumbusha hesabu hizi,cha
kufanya ni wewe kujua idadi ya kozi zako huko SARMS zipo ngapi? Kwa mfano
tufanye zipo 5
d)
Baada ya kujua madaraja ya kila kozi huko SARMS
mf: kozi1 una A ,kozi2 una C,kozi 3 una B+,kozi 4 una B na kozi5 una A.
e)
Si unakumbuka pointi za madaraja? Jikumbushe kipengele (a) hapo
juu,umekumbuka eeeh! Jiulize una A ngapi katika kozi zako tano? Kwa mujibu wa
matokeo una A mbili,basi fanya (2 mara 5=10),una B+ ngapi? Hapo inaonekana moja
tu,basi fanya (1 mara 4=4),una B mbili (2 mara 3=6) na mwisho una C mija (1
mara 2=2).
f)
Sasa tunaanza kutafuta jumla ya pointi kwa
tano,ambapo kwenye A kuna pointi 10,B+ kuna pointi 4,B kuna pointi 6 na C kuna
pointi 2.
Jumla=10+4+6+2
=22
Sasa hapa unaweza kupata GPA yako kwa kuchukua jumla ya pointi ugawanye kwa
idadi ya kozi ambazo ni tano tu
=22/5
GPA=4.4
TEMBELEA KILA SIKU KWA HABARI MAKINI SANA
No comments:
Post a Comment
Comment here