Kumekuwapo na picha ambazo zimesambaa
kuhusu ajali inayodaiwa kuhusisha basi la kampuni ya Ngorika na lingine
la Ratco kwamba yamegongana uso kwa uso. Millardayo.com imempata kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Bonaventure Mushongi na ameeleza haya……
>>> ‘mpaka
sasa hivi kulingana na mimi nilivyofuatilia bado sijaona, tumejaribu
kufuatilia kila hatua, hawa waliotuma wanaweza wakatusaidia lakini mpaka
sasa hivi kulingana na taarifa zangu za barabarani sina taarifa hizo
mpaka sasa hivi’
>>>’hali
hii inatisha watu, unajua siku mbili tatu kumekuwa na ajali za kutisha
hivyo unapoongelea vitu vingine unasababisha taharuki, ningeliomba
tusitumie vibaya mitandao hii kwa sababu sheria ziko wazi’
No comments:
Post a Comment
Comment here