Monday, July 4, 2016

MOUNT MERU OFFICIAL.





                                  MOUNT MERU UNIVERSITY OFFICIAL

              


               MITIHANI YA KUMALIZA MHULA WA PILI 2015/2016
                                                  (MOUNT MERU UNIVERSITY)
                                   KUANZA MAPEMA JUMATATU HII.

Wanafunzi wa Chuo kikuu cha mount meru mkoani arusha,(leo) jumatatu wataaza mitihani yao ya kumaliza mhula wa pili. Aidha mitihani hii itafanyika ndani ya wiki mbili (kuanzia tar 4/7/2016-18/7/2016) na baadae wanachuo hao kutawanyika katika maeneo mbalimbali ambako watafanya mazoezi ya kile walichovuna kwa mwaka mzima. Mazoezi hayo maarufu (TP) yatakuwa ni maalumu kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na mwaka wa pili tofauti na mwaka wa tatu ambao wakimaliza mtihani watalazimika kusubiri mpaka mwezi oktoba ili kufanya mahafari.

                     bED ONE WALIA NA RATIBA YA MTIHANI.

Kwa upande mwingine ratiba imeonekana kuwa ni ngumu kwa wanafunzi wa BED ONE maana wiki ya kwanza wana mtihani mmoja na wiki ya pili ikiwa mitihani minane.
Waziri wa elimu alisema
 “ratiba kama hii haiepukiki maana ofisi imezingatia sikukuu ya IDD na sikukuu ya sabasaba na kalenda ya masomo kwa ujumla”.
Kwa upande wake kiongozi wa BED ONE (CR), amevunja ukimya na kunena yafuatayo 
“ratiba ni ngumu ila ni ratiba rafiki kwa waliosoma”.

                          OFISI YAONYA.

Utawala umetoa mwongozo kuwa madarasa yatayotumika ni HA4, HA5, HA6 NA HA7. Hivyo mwanachuo anapashwa kufika muda mwafaka akiwa na kitambulisho na PASSBOOK na aketi sehemu aliyopangwa.
Maonyo mengine ambayo ofisi imetoa ni kama,
1.     Kaa sehemu palipo na namba yako ya usajili vinginevyo hutafanya mtihani.
2.     Kama passbook yako haijasainiwa katika ule ukurasa wa kijani, utatolewa nje ya mtihani.
3.     Ukikamatwa na nyaraka zozote ambazo huruhusiwi kuingia nazo kwenye chumba cha mtihani, utatolewa ndani ya chumba cha mtihani na hautaruhusiwa kabisa kuendelea na mitihani.
4.     Ukionekana umebadili ama kutoa namba yako ya mtihani sehemu ilipo, hautaruhusiwa kuendelea na mitihani mingine.
Aidha ofisi imesisitiza kila mhusika kuzingatia taarifa hizi.

             UFAFANUZI KUHUSU MASUALA YA FIELD

Waziri mwenye kandarasi ya mikopo chuoni, amesema lipo tumaini kubwa la watu kupata pesa yao ya FIELD kabla hawajaondoka. “Zoezi la upatikanaji wa pesa ya field liko hatua za mwisho, watu watapewa pesa yao kabla hawaondoka na hata kama ikitokea tumemaliza mitihani na bado pesa haipo, basi mimi nitakuwa wa mwisho kuondoka hapa” alisema waziri.
Katika upande mwingine kuna watu ambao majina yao hayakuonekana kwenye orodha ya wanafunzi watakaofanya field sehemu mbalimbali kuanzia mapema mwezi august, Waziri wa elimu amefuatilia , awali ilikuwa watu hao wangepangiwa kufanya field shule ya MAGRETH , Lakini DVC AA ametoa mkono wa neema walau watu hao wafanye field sehemu na shule yoyote ndani ya mkoa wa arusha. Siku ya ijumaa DVC AA atatoa tena tamko la mwisho ambalo ndio litakuwa barikio la zoezi zima.



                                                                                      Dr west


No comments:

Post a Comment

Comment here