
ARUSHA
RAIS John Magufuli ametoa wito kwa
Watanzania kumuombea ili aendelee kuwashughulikia wote wanaofanya
ubadhirifu wa fedha za umma kupitia kampeni yake ya kutumbua majipu.
“Nataka
niwahakikishieni kuwa nitaendelea kutumbua majipu yote mpaka yaishe, na
naomba mniombee ili kazi hii ya kutumbua majipu ifanyike kwa
mafanikio,” alisema Dk Magufuli.

Alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa
akizungumza na wananchi katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha jana,
alipotua kwa ziara ya kikazi ikiwa ni ya kwanza kwao tangu achaguliwe
kushika wadhifa huo Novemba 5, mwaka jana.
Dk
Magufuli aliwasili mkoani Arusha, ambako kesho atatunuku Kamisheni kwa
maofisa wanafunzi wa kundi la 57/15 katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi
(TMA) Monduli mkoani hapa.

Rais Magufuli aliwasili mjini Arusha
akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), alikotua kwa
ndege akitokea jijini Dar es Salaam na kupokewa na mamia ya wananchi.
Akiwa uwanjani hapo, Rais Magufuli aliwashukuru wananchi kwa mapokezi
makubwa aliyoyapata na aliwaeleza kuwa uchaguzi umekwisha, kilichobaki
ni kazi tu.
“Nawashukuru
sana ndugu wananchi kwa mapokezi haya makubwa, naomba kuwahakikishia
kuwa uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kuchapa kazi tu,” alisema Rais Magufuli.

Akiwa njiani kutoka KIA, Rais Magufuli
alisimamishwa na wananchi wa njiapanda ya KIA, Kikatiti, Usa River,
Tengeru na Mount Meru mjini Arusha ambako huko kote pamoja na kusisitiza
kuwa uchaguzi umekwisha na kilichobaki ni kuchapa kazi, aliwahakikishia
kuwa hatawaangusha.
Aidha,
Rais Magufuli alisema tayari serikali imeanza kutoa fedha kwa ajili ya
kugharimia elimu ya msingi na sekondari baada ya kufuta ada na alionya
kuwa watumishi wa umma hususani wakuu wa shule watakaothubutu kufanya
ubadhirifu wa fedha hizo watashughulikiwa.
Alisema
yote aliyoyaahidi kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na Watanzania kwa
ujumla, ikiwemo ujenzi wa barabara za Arusha, kulipa fidia za wananchi
na kufuta ada ya shule za msingi na sekondari yanatekelezwa.
Rais
Magufuli alisisitiza kuwa serikali yake haitawabagua Watanzania kwa
dini zao wala makabila yao na wala haitawabagua kwa misingi ya vyama
vyao na kanda zao. Aliwataka Watanzania wote kuiweka mbele Tanzania na
kushirikiana kuiendelez



No comments:
Post a Comment
Comment here