NEWS ALERT: TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR YATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI
ZANZIBAR
Tume yatangaza tarehe ya uchaguzi Zanzibar.
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)
imetangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi visiwani humo baada ya matokeo
ya uchaguzi uliopita kufutwa.
Uchaguzi huo sasa utafanyika Jumapili tarehe 20 Machi.
Tangazo hilo limefanywa na mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha.
Bw Jecha amesema tarehe hiyo iliamuliwa na tume baada ya mkutano hapo jana.
“Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa
Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na hakutakuwa na
uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni,” amesema Bw Jecha.
“Wagombea wote walioteuliwa hapo awali wataendelea kuwa wagombea katika uchaguzi huu.”
No comments:
Post a Comment
Comment here